Palikuwa na wakati ambapo kulikuwa na jua saba angani. Kwa sababu ya joto jingi, watu wanaamua kuziondoa jua zote. Wanaenda mbali zaidi na hatimaye, ni jogoo ndiye anayeiokoa siku.
Mvulana aliyekuwa na sura mbaya anaenda msituni kutafuta mzizi wa kipekee ambao mwanamke mkongwe wa kiajabu anaahidi utamwezesha kuwa wa kupendeza. Kule msituni anakumbwa na majaribu mengi.
Nyanya anamshonea mjukuu wake mdogo sketi nzuri ya kupendeza. Marafiki zake wanaona wivu hivyo wanampangia njama kwa nia ya kujipatia ile sketi. Kisha msichana anamezwa na nyoka. Kwa bahati nzuri, nyanyake anamwokoa.
Wasichana watatu wadogo wanakutana na jitu ambalo lajifanya kutaka msaada wao. Wakati jitu linamwongoza msichana mmoja mbali mtu mmoja anawasimamisha na kuuliza jina la msichana yule. Nini kitakachotokea kwa msichana huyo?
Wavulana wawili wanaopenda kuchunguza mazingira yao wanaishia kupitia yale ambayo hawakuwahi fikiria ingetendeka kwao. Soma uone ilivyokuwa!
Kulikuwa na mvulana mdogo asiyeweza kutenda jambo lolote vyema. Mamake alimvumilia, lakini babake hakuweza kumstahimili. Siku moja babake aliamua kumfukuza kutoka nyumbani kwake. Mama alienda na mtoto wake. Nini kilitokea kwa Kisirusiru na mamake?
By navigating this website, you agree to the storing of cookies on your device to enhance site navigation and analyze site usage.