Urafiki baina ya fisi na kunguru unakatika baada ya kunguru kumdanganya fisi. Soma uone vipi hili lilitokea.
Wavulana wawili wanaopenda kuchunguza mazingira yao wanaishia kupitia yale ambayo hawakuwahi fikiria ingetendeka kwao. Soma uone ilivyokuwa!
Msichana mdogo anatazama na kudadizi namna bibi yake anavyotayarisha kuziweka ndizi ili ziive. Anakoziweka ndizi inabaki siri kubwa kwa huyu msichana anaudhika na jambo hilo. Je, inachukuwa muda gani kabla msichana yule kuitambua siri ya bibi?
Hadithi ya mapenzi yenye huzuni kumhusu binti mrembo wa kifalme anayeamua kufuata moyo wake badala ya alivyotaka babake.
Mvulana aliyekuwa na sura mbaya anaenda msituni kutafuta mzizi wa kipekee ambao mwanamke mkongwe wa kiajabu anaahidi utamwezesha kuwa wa kupendeza. Kule msituni anakumbwa na majaribu mengi.
Nyanya anamshonea mjukuu wake mdogo sketi nzuri ya kupendeza. Marafiki zake wanaona wivu hivyo wanampangia njama kwa nia ya kujipatia ile sketi. Kisha msichana anamezwa na nyoka. Kwa bahati nzuri, nyanyake anamwokoa.
By navigating this website, you agree to the storing of cookies on your device to enhance site navigation and analyze site usage.